Maradhi ya Sajuki, laana kwa Steps Entertainment
Haiwezekani Sajuki awafuate akiwa anaumwa, awaombe msaada wao wamjibu kwamba aende akarekodi filamu, awapelekee waiuze ndiyo zipatikane fedha za kumsafirisha kwenda India kwenye matibabu. Jamani huyu mtu kawafuata anaumwa, hali yake haijifichi, anaumwa kweli lakini kajibiwa hivyo.
Tuone sasa umoja wa wasanii. Nangoja kusikia misimamo ya Vincent Kigosi ‘Ray’, Jacob Steven ‘JB’, Single Mtambalike ‘Richie’ na wengine, kuhusu kujiondoa Steps kutokana na kile ambacho amefanyiwa Sajuki. Ni hatua muhimu kama watafanya hivyo, kwani watakuwa wameitetea tasnia.
Kinyume chake itakuwa ni unafiki. Usaliti, ubinafsi, kuendekeza njaa na kusahau utu. Leo lipo kwa Sajuki, hakuna kati yetu anayejua nani kesho atakuwa mgonjwa pengine kuliko huyo mwenzetu. Kama ndivyo, basi hatutakiwi kupandisha mabega, kwani tafsiri ya kesho ipo kwa Mungu peke yake.
Haishindikani kufanya kazi na makampuni mengine. Inawezekana pia kwa umoja wenu mkaanzisha mtandao wa kusambaza na kuuza kazi zenu. Hili litawapa heshima kubwa kwa kujikomboa, vilevile kushiriki kwa ari na nguvu kupambana na udhalilishaji aliofanyiwa mwenzao.
Hili si la kupuuza, kuna leo na kesho. Usingoje nawe likufike ndiyo ufundishwe kwa mtindo wa kusutwa. Kwamba umeona sasa, enzi zile alipofanyiwa Sajuki uliona sawa, leo yamekufika na wewe ndiyo unaumia. Ni tahadhari tu kwa sababu hii dunia hatuimiliki, kwa hiyo hatuna budi kutendeana haki.
Maisha yetu na tafsiri ya mkate wa kila siku ni mtihani, hivyo kugoma kupeleka kazi Steps inawezekana ni jambo zito. Kama ndivyo, basi tuone kauli zenu za kuonesha kuchukizwa na uamuzi wa kampuni hiyo dhidi ya Sajuki. Toeni sauti basi, mkikaa kimya tutawaona waoga, wazandiki, wanafiki msiojali utu mbele ya fedha.
Tatizo la Steps baada ya kulitazama katika muktadha mpana ni upungufu wa utu mbele ya fedha. Hivyo, hata wasanii watakaokubali kuendelea kufanya kazi na kampuni hiyo, watakuwa hawana ubinadamu. Kwa maana wao wapo radhi mwenzao atoswe, anyanyaswe na kadhalika bila wao kuguswa kwa chochote.
Mimi siyo mtabiri lakini ukweli ukae kwenye kipimo chake kwamba historia itawahukumu. Taadhira na manyanyaso aliyofanyiwa Sajuki haviwezi kupita kimya. Ray na wenzako, zindukeni leo, semeni hapana kwa hili alilotendewa Sajuki. Mafanikio mtayaona hapa duniani na kesho ahera.
Steps imejitengenezea sifa mbaya. Leo hii Sajuki ana mtoto, atakapokua na kujua baba yake aliambiwa afanye kazi ndiyo apate fedha za matibabu wakati hajiwezi, chuki itakaa na akiwa mtu wa kinyongo, ataieneza kwa kizazi chake chote. Namuombea sana maisha marefu Sajuki.
Wakati unasoma makala haya, pengine picha za aina tofauti zinaweza kuingia kichwani kwako na kutoka lakini kubwa ni moja tu, Sajuki anaumwa, yupo dhoofu, anahitaji kusaidiwa lakini wenye upungufu na utu, wamemwambia aende akafanye kazi. Eti, asiporekodi filamu atakufa na maradhi yake.
Ni kwa nini Steps wasingewekeza kwa Sajuki, wakampeleka India kwenye matibabu? Mbona baada ya kupona angefanya kazi nzuri, tena kwa umakini mkubwa? Hapo bila shaka angekuwa na shukurani nyingi juu ya Steps, kwa hiyo angefanya kazi yake yenye nguvu ili kulipa fadhila.
Sajuki anaumwa, tena anaumwa hasa. Anahitaji msaada wa hali na mali ili atibiwe na kurejea kwenye afya yake. Naomba nisisitize, msanii huyo anaumwa kwelikweli na anahitaji matibabu ya haraka. Fedha zinahitajika akatibiwe India. Huko ndiko kwenye tiba yake.
Pamoja na moyo wa kujitolea ambao mtu yeyote anaweza kuwa nao, hivyo kumchangia kama siyo kumuwezesha Sajuki kwenda India kutibiwa, Steps ilipaswa kuwa ya kwanza, ama kwa kumchangia au kuwezesha safari ya nchi hiyo. Leo tungekuwa tunazungumza mengine lakini thubutu!
Nasema Steps ilipaswa kuwa ya kwanza kwa sababu yenyewe ndiyo inayouza filamu za Sajuki. Kampuni hii inajua matunda ya msanii huyo. Angalau ingefanya hivyo kuonesha namna ilivyoguswa na matatizo ya ndugu yetu. Kama sivyo hivyo, basi uungwana tu.
Steps wanatambua kwamba Sajuki anaumwa lakini wamemfanyia vitendo vya uvunjifu wa haki za binadamu. Wamemtesa kwa kumtumikisha kazi ilhali wanatambua kwamba anaumwa. Tena maradhi ambayo yanahitaji utulivu na faraja. Jamani Sajuki anaumwa, tuache utani, tumuombee, tumchangie akatibi
No comments:
Post a Comment