Mgimwa awakuna wabunge
WAZIRI
wa Fedha, Dk. William Mgimwa ‘amewakuna’ wabunge wa Bunge la Tanzania
baada ya kuwajulisha kuwa Serikali imekubali mapendekezo yao mengi
waliyotoa wakati wanachangia bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha
2012/2013.
Miongoni mwa mapendekezo ya
wabunge yaliyokubaliwa ni kuongeza kima cha chini cha mapato ya
wafanyabiashara yanayotozwa kodi kutoka shilingi milioni tatu hadi
milioni nne.
Dk. Mgimwa
amelieleza Bunge kuwa, uamuzi huo wa Serikali utawawezesha
wafanyabiasha wadogo wakiwemo waendesha ‘bodaboda’ kujiendeleza
kibiashara.
Serikali yetu ya
Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni sikivu…Serikali ni sikivu kwa wabunge
wote” amesema Dk. Mgimwa wakati anajibu hoja za wabunge waliochangia
bajeti hiyo.
Amewaeleza wabunge
kuwa, Serikali pia imekubali ushauri wao wa kuongeza kodi ya mafuta kwa
mafuta yanayoagizwa kutoka nje ili kulinda viwanda vya ndani. Kwa
mujibu wa Waziri Mgimwa, uamuzi huo wa Serikali sasa utawasilishwa
kwenye Baraza la Mawaziri na nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki(EAC).
“Lakini Serikali
imekubali mapendekezo ya waheshimwa wabunge” amesema. Kwa mujib wa
Waziri Mgimwa, Serikali kuondoa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwa
viwanda vinavyozalisha nguo kwa kutumia pamba inayolimwa nchini.
“Tumeikubali
hiyo hoja, tunaifanyia kazi” amelieleza Bunge na kubainisha kwamba,
uamuzi huo utasaidia kuongeza ajira nchini na mapato ya wananchi.
Amesema,
Serikali inafanya uchambuzi wa suala hilo ili kuona ni wapi itafidia ,
nakwamba, itatoa ufafanuzi wa jambo hilo katika Muswada wa Fedha
wakati wa Mkutano unaoendelea wa Bunge mjini Dodoma.
MATUKIO YA PICHA KUTOKA BUNGENI DODOMA LEO
CTR YAKUBALI KUHAMISHA KESI YA RYANDIKAYO
Na Ashura Mohamed-Arusha
Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) Jumatano imekubali maombi ya mwendesha mashitaka wa mahakama hiyo ya kuhamishia kesi ya mtuhumiwa wa mauaji ya kimbari ambaye bado anasakwa, Charles Ryandikayo,kwenda kusikilizwa nchini Rwanda, ikiwa kesi ya sita kuhamishiwa nchini humo.
Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) Jumatano imekubali maombi ya mwendesha mashitaka wa mahakama hiyo ya kuhamishia kesi ya mtuhumiwa wa mauaji ya kimbari ambaye bado anasakwa, Charles Ryandikayo,kwenda kusikilizwa nchini Rwanda, ikiwa kesi ya sita kuhamishiwa nchini humo.
Mahakama
iliyotoa maamuzi hayo ikiongozwa na Jaji, Vagn Joensen imeeleza
kwamba, kwa kuzingatia hoja zilizowasilishwa na pande zote mbili,
imefikia uamuzi wa kuhamishia kesi hiyo nchiniRwanda.
‘’Mahakma
imeamua kesi kupelekwa kwenye mamlaka ya Jamhuri yaRwandaili wenye
mamlaka hayo kuiwasilisha kesi hiyo mbele ya Mahakama Kuu yaRwandakwa
ajili ya kuanza kusikilizwa kwa haraka,’’ inasomeka sehemu ya uamuzi
huo.
Imeelezea
matumaini yake kwamba’’Jamhuri yaRwanda, kwa kukubali kupokea kesi
kutoka mahakama hiyo ya Umoja wa Mataifa, itatimiza wajibu wake kwa
uaminifu, uwezo na nia njema ya kuendesha kesi hiyo kwa kufuata viwango
vya juu vya haki vya kimataiafa.’
’
Ryandikayo
ambaye alikuwa Meneja wa mgahawa mmoja wa Mubuga katika wilaya ya
Gishyita mkoani Kibuye, Magharibi yaRwandaanashitakiwa kwa mauaji ya
kimbari, kula njama za kufanya mauaji hayo, uhalifu dhidi ya binadamu
na uhalifu wa kivita.ICTR imeshatoa maamuzi katika maombi
matanokamahayo.
Maombi
hayo yanahusu mtu mwingine ambayo bado anasakwa pia, Ladislas
Ntaganzwa, meya wa zamani wa wilaya ya Nyakizu, mkoani Butare, Kusini
mwaRwandana Bernard Munyagishari, anayedaiwa kuwa kiongozi wa wanamgambo
wa Interahamwe mkoa wa Gisenyi, Kaskazini ya Rwanda.Lakini upande wa
utetezi unatarajiwa kupinga maamuzi hayo.
Maombi
mengine matatu ya aina hiyo ambayo yameshatolewa uamuzi na ICTR
yanawahusu, Mchungaji Jean Uwinkindi na watuhumiwa wawili ambao nao
bado wanasakwa ikiwa ni pamoja na Fulgence Kayishema na Charles
Sikubwabo.
Maombi
mengine mawili ya aina hiyo ambayo yapo mbele ya mahakama yakisubiri
uamuzi ni pamoja na ya Aloys Ndimbati, meya wa zamani wa Gisovu na
Luteni Kanali Pheneas Munyarugarama, kamanda wa zamani wa kambi ya
jeshi ya Gako, wilayani Kanzenze katika mkoa wa Kigali Vijijini.
John Mnyika akitoka nje ya Bungeni
Mbunge
wa jimbo la Ubungo John Mnyika akitoka katika ukumbi wa Bunge la
Tanzania jana mjini Dodoma baada ya kukataa kufuta kauli ya
kumdhalilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa dhaifu.
Mbunge huyo alitoa kauli hiyo wakati akichangia Bajeti ya serikali ya
mwaka 2012/13 katika mkutano unaoendelea.MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA KULA CHAKULA CHA JIONI NA VIONGOZI WA UMOJA WA WATANZANIA WAISHIO NCHINI BRAZIL
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akizungumza jambo na Katibu wa Umoja wa Watanzania, waishio
nchini Brazil, Heri Juma Mbwana, wakati alipokutana nao katika hafla ya
chakula cha jioni na mazungumzo, iliyofanyika katika Hoteli ya Arena,
Rio de Jeneiro, jana Juni 22, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akizungumza jambo na mmoja kati ya wajumbe wa Umoja wa
Watanzania, waishio nchini Brazil, , wakati alipokutana nao katika hafla
ya chakula cha jioni na mazungumzo, iliyofanyika katika Hoteli ya
Arena, Rio de Jeneiro, jana Juni 22, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, Mke wa Makam wa Rais, Mama Zakhia Bilal,Naibu Waziri wa Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maadhi Juma Maalim, Balozi wa Tanzania
nchini Brazil Francis Malambugi, na Balozi Liberata Mulamula, wakiwa
katika picha ya pamoja na Viongozi wa Umoja wa Watazanaia, wakati
alipokutana nao viongozi hao wa moja wa Watanzania, waishio
nchini katika hafla ya chakula cha jioni na mazungumzo, iliyofanyika
katika Hoteli ya Arena, Rio de Jeneiro, jana Juni 22, 2012. Picha na
Muhidin Sufiani-OMR
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akizungumza Viongozi wa Umoja wa Watanzania, waishio nchini
Brazil, wakati alipokutana nao katika hafla ya chakula cha jioni na
mazungumzo, iliyofanyika katika Hoteli ya Arena, Rio de Jeneiro, jana
Juni 22, 2012. Kulia ni Mama Zakhia Bilal (kushoto) ni Balozi
wa Tanzania, nchini Brazil, Francis Malambugi. Picha na Muhidin
Sufiani-OMR
|
No comments:
Post a Comment