Tuesday, June 26, 2012

Mahakama Kuu ya Tanzania imetoa amri ya kusitisha mgomo wa Madaktari

Kufuatia Tangazo la Chama cha Madaktari nchini (MAT) la kuanza mgomo siku ya Jumamosi tarehe 23 Juni, 2012, Mahakama Kuu ya Tanzania,Kitengo cha kazi,Dar es Salaam imetoa amri ya kusitisha mgomo huo mpaka hapo pande zote mbili yaani Serikali na Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) yatakaposikilizwa na kutolewa uamuzi.
·         Amri hiyo ya Mahakama imetolewa kufuatia maombi namba 73 ya 2012 yaliyowasilishwa chini ya hati ya dharura na Mwanasheria Mkuu wa Serikali dhidi ya Chama cha Madaktari Tanzania (MAT).Sababu za msingi amabazo zimepelekea Mahakama kuu kutoa amri hiyo upande mmoja ni pamoja na;
·         Iwapo mgomo huo utatokea utakuwa na kuwa amri hii isipotolewa madhara yake ni makubwa isiyoweza kufidiwa kwa namna yoyote ile kama vile kupoteza maisha n.k
·          Wajibu maombi,ambao ni MAT, inaundwa na Madaktari ambao wapo katika Sekta ambayo inatoa huduma mahsusi (essential service sector), Aidha Chama cha Madaktari Tanzania kimetangaza mgomo bila kufuatia taratibu zilizoanishwa katika Kifungu cha 76(1 na 2) cha Sheria ya Kazi (Employment and Labour Relations Act No 6 ya 2004.
Masharti hayo ni
·         Kuzuia wafanyakazi walio katika Sekta Muhimu kugoma na kama wakigoma,
·         Kuwepona makubalianao ya pamoja ya kutoa huduma za msingi wakati mgomo ukiendelea.
Kwa misingi hii,Mahakama Kuu ya Tanzania, kwa Chama cha Madktari Nchini na wanachama wake kusitisha na kutoshiriki katika mgonmo huo.

Friday, June 22, 2012

FRANK DOMAYO KUTOKA U 20 ATUA YANGA


Mchezaji mpya wa Timu ya Dar-young African aliyekuwa akichezea timu ya taifa ya umri chini ya miaka 20 Ngorongoro Heroes FRANK DOMAYO,ameanza rasmi mazoezi na timu yake mpya yenye maskani yake mtaa wa Jangwani na Twiga katika uwanja wa Kaunda Jijini Dar-es-salaam.
DOMAYO ambaye ameonesha jitihada kubwa katika mazoezi hii leo, amekuwa kivutio kikubwa kwa mashabiki wa timu hiyo pamoja na aliyekuwa beki wa wapinzani wao KELVIN YONDANI ambaye usajili wake ulizua utata hivi karibuni baina ya Timu hizo kongwe nchini.

MISRI YAOMBA KUIKABILI NGORONGORO HEROES


Chama cha Mpira wa Miguu Misri (EFA) kimeomba mechi mbili za kirafiki kwa timu yao ya vijana na timu ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 ya Tanzania (Ngorongoro Heroes).
EFA imeomba mechi hizo zichezwe Julai 3 na Julai 5 mwaka huu kwa masharti maalumu. Ikiwa zitachezwa Misri, mwenyeji (EFA) atagharamia Ngorongoro Heroes kwa malazi, chakula, usafiri wa ndani na sehemu ya kufanyia mazoezi.
Ikiwa mechi hizo zitachezwa Dar es Salaam, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) litaigharamia timu ya Misri kwa malazi, chakula, usafiri wa ndani na sehemu ya mazoezi. Hivyo kila timu itajigharamia kwa usafiri wa ndege na posho kwa timu yake.
Sekretarieti ya TFF inafanya uchambuzi wa gharama ili kujua ipi ni nafuu kabla ya kufanya uamuzi wa wapi mechi hizo zichezwe.
Ngorongoro Heroes imeingia raundi ya pili ya michuano ya Afrika ambayo fainali zake zitafanyika mwakani nchini Algeria baada ya kuitoa Sudan katika raundi ya kwanza.
Itacheza mechi ya kwanza ya raundi ya pili Julai 28 mwaka huu jijini Dar es Salaam wakati ya marudiano itakuwa Agosti 11 mwaka huu nchini Nigeria.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

TFF:AWAMU YA KWANZA USAJILI MWISHO AGOSTI 10






Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)




Kipindi cha kwanza cha usajili wa wachezaji kwa ajili ya msimu wa 2012/2013 kitamalizika Agosti 10 mwaka huu kulingana na kalenda ya Matukio ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ya 2012/2013.
Uhamisho wa wachezaji unafanyika kuanzia Juni 15 hadi Julai 30 mwaka huu wakati kipindi cha kuacha wachezaji (sio wa Ligi Kuu. Wachezaji wa Ligi Kuu wanacheza kwa mikataba) ni kuanzia Juni 15- 30 mwaka huu.
Kwa klabu za Ligi Kuu kutangaza wachezaji watakaositishiwa mikataba yao ni kuanzia Juni 15-30 mwaka huu na usajili wa wachezaji unafanyika kuanzia Juni 15 hadi Agosti 10 mwaka huu.
Tunasisitiza kipindi cha usajili kiheshimiwe na mikoa yote kwa sababu usajili huo huo ndiyo utakaotumika katika michuano ya Kombe la FA. Kwa maana nyingine hakutakuwa na kipindi kingine cha usajili wa wachezaji kwa klabu zote nchini hadi hapo litakapofunguliwa dirisha dogo.
Mechi ya kufungua msimu ya Ngao ya Jamii (Community Shield) kati ya mabingwa wa Ligi Kuu, timu ya Simba na makamu bingwa Azam itachezwa Agosti 25 mwaka huu wakati Ligi Kuu itaanza Septemba Mosi mwaka huu, na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) yenyewe itaanza Septemba 15 mwaka huu.
Ratiba ya Ligi Kuu itatolewa Julai 23 mwaka huu.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AIWAKILISHA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA UMOJA WA MATAIFA KUHUSU MAZINGIRA ENDELEVU JIJINI RIO DE JANEIRO-BRAZIL


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwasili kwenye Viwanja vya Ukumbi wa Mikutano, wakati alipofika kuiwakilisha nchi katikaMkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mazingira Endelevu (Rio+20) jana Juni 21, jijini Rio de Janeiro, nchini Brazil. Mkutano huo ni wa pili kufanyika nchini hapa tangu ulipofanyika kwa mara ya kwanza mwaka 1992. Kushoto kwake ni Balozi wa Tanzania nchini Brazil, Francis Malambugi. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia katika Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mazingira Endelevu (Rio+20) jana Juni 21, jijini Rio de Janeiro, nchini Brazil. Mkutano huo ni wa pili kufanyika nchini hapa tangu ulipofanyika kwa mara ya kwanza mwaka 1992. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Dkt. Terezya Huvisa, Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa rais wa Zanzibar, Fatma Fereji, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mahadhi Juma Maalim, wakiwa katika Ukumbi wa mkutano, wakati walipohudhuria mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mazingira Endelevu (Rio+20) jana Juni 21, jijini Rio de Janeiro, nchini Brazil. Mkutano huo ni wa pili kufanyika nchini hapa tangu ulipofanyika kwa mara ya kwanza mwaka 1992. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa rais wa Zanzibar, Fatma Fereji, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mahadhi Juma Maalim, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Dkt. Terezya Huvisa. wakiwa katika mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mazingira Endelevu (Rio+20) jana Juni 21, jijini Rio de Janeiro, nchini Brazil. Mkutano huo ni wa pili kufanyika nchini hapa tangu ulipofanyika kwa mara ya kwanza mwaka 1992. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
 Balozi Liberata Mulamula, na Balozi wa Tanzania, nchini Brazil,Francis Malambugi, wakiwa katika mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mazingira Endelevu (Rio+20) jana Juni 21, jijini Rio de Janeiro, nchini Brazil. Mkutano huo ni wa pili kufanyika nchini hapa tangu ulipofanyika kwa mara ya kwanza mwaka 1992. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

Balozi Liberata Mulamula, akifurahia jambo baada ya kukutana na Wabunge wa Tanzania, (kushoto) ni Mbunge wa (wa pili kushoto) ni Mbunge wa Kahama Bw. James Lembeli, (wa pili kulia) ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Sazi Salula, (katikati) ni Mkurugenzi wa mazingira, Ofisi ya Makamu wa rais, Dkt.Julius Ningu, katika Viwanja vya Kumbi za mikutano ya Rio+20, wakati walipofika kuhudhuria mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mazingira Endelevu (Rio+20) jijini Rio de Janeiro, nchini Brazil. Mkutano huo ni wa pili kufanyika nchini hapa tangu ulipofanyika kwa mara ya kwanza mwaka 1992. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia katika Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mazingira Endelevu (Rio+20) jana Juni 21, jijini Rio de Janeiro, nchini Brazil. Mkutano huo ni wa pili kufanyika nchini hapa tangu ulipofanyika kwa mara ya kwanza mwaka 1992. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

RAIS AREJEA TOKA DODOMA LEO

YONDANI ATUA YANGA

Awa kivutio mazoezini"
"Gazeti moja laumbuka kwa propaganda za Simba"
"Kisa eti ametekwa na Simba"
Hatimaye aliyekuwa beki wa kutumainiwa wa klabu ya Simba katika msimu uliopita Kevin Yondan "Vidic" leo amekata mzizi wa fitina baada ya kuanza rasmi mazoezi  katika uwanja wa Kaunda uliopo Makao Makuu ya klabu ya Yanga na kuwa kivutio katika mazoezi hayo.
Kipenzi hicho cha Yanga kiliwasili majira ya saa tatu kasoro dakika kumi asubuhi, ambapo mara baada ya kushuka katika gari mashabiki waliofurika katika mazoezi hayo walipomuona ghafla walimshangilia kwa vifijo na nderemo huku akielekea uwanjani akiwapungia mashabiki hao mikono.
Vidic ambaye ana mapenzi makubwa na klabu ya Yanga, leo ameripotiwa na chombo  kimoja cha  habari kuwa eti alitekwa hapo jana  na klabu ya Simba na kudaiwa kushiriki katika mazoezi na timu yake hiyo ya zamani.

Kelvin Yondan
 
Mchezaji huyo ambaye kila kukicha timu yake hiyo ya zamani ikiendelea kumuota kwa mazuri aliyowafanyia amekuwa gumzo kwa kipindi hiki cha usajili ambapo timu yake mpya ya Yanga ikiendelea kufanya kufuru ya usajiri ambao unatarajiwa kumalizika Julai 15 Mwaka huu.
Yondan hivi karibuni aliwashukuru wanachama na wapenzi wa klabu ya  Simba kwa ushirikiano aliokuwa akiupata wakati akiitumikia timu hiyo,aliweka bayana mara baada ya kumwaga wino kuichezea Klabu ya Yanga kuwa Simba isihangaike na yeye kwakuwa hana mpango tena wa kuichezea klabu yake ya zamani.
 
Katika hali isiyokuwa ya kawaida mwanachama mmoja wa klabu ya Simba kwa jina maaraufu (Kobe) muda mfupi uliopita wakati www.youngaficans.co.tz ikiwa mitamboni aliwasili katika mazoezi ya timu ya Yanga yaliyokuwa yakifanyika katika uwanja wa Kaunda kwa ajili ya kutaka kuhakikisha juu ya uvumi wa beki Kevin Yondan kuwa yupo katika mazoezi.
 


Mara baada ya kumshuhudia mchezaji huyo akifanya mazoezi mwanachama huyo aliangua kilio uwanjani hapo huku mashabiki wa Yanga wakishangilia na kumnunulia maji ya matunda pamoja na uji.
 
Wachezaji wengine walioanza mazoezi leo ni pamoja na kiungo wa timu ya Taifa Frank Domayo aliyekuwa JKT Ruvu na mshambuliaji wa timu ya Taifa  Saimon Msuva aliyekuwa Moro United.
 
Naye Kocha msaidizi wa Klabu ya Yanga Fredy Felix Minziro amesema kikosi chake chote  kinatarajiwa kukamilika mara baada ya wachezaji Haruna Niyonzima aliyekuwa na timu ya Taifa lake(Rwanda) na Rashid Gumbo anayeumwa malaria watakapojiuunga na kikosi hicho.Habari kwa hisani ya http://www.youngafricans.co.tz

Mgimwa awakuna wabunge

WAZIRI wa Fedha, Dk. William Mgimwa ‘amewakuna’ wabunge wa Bunge la Tanzania baada ya kuwajulisha kuwa Serikali imekubali mapendekezo yao mengi waliyotoa wakati wanachangia bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2012/2013.

Miongoni mwa mapendekezo ya wabunge yaliyokubaliwa ni kuongeza kima cha chini cha mapato ya wafanyabiashara yanayotozwa kodi kutoka shilingi milioni tatu hadi milioni nne.
Dk. Mgimwa amelieleza Bunge kuwa, uamuzi huo wa Serikali utawawezesha wafanyabiasha wadogo wakiwemo waendesha ‘bodaboda’ kujiendeleza kibiashara.
Serikali yetu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni sikivu…Serikali ni sikivu kwa wabunge wote” amesema Dk. Mgimwa wakati anajibu hoja za wabunge waliochangia bajeti hiyo.
Amewaeleza wabunge kuwa, Serikali pia imekubali ushauri wao wa kuongeza kodi ya mafuta kwa mafuta yanayoagizwa kutoka nje ili kulinda viwanda vya ndani. Kwa mujibu wa Waziri Mgimwa, uamuzi huo wa Serikali sasa utawasilishwa kwenye Baraza la Mawaziri na nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC).
 “Lakini Serikali imekubali mapendekezo ya waheshimwa wabunge” amesema. Kwa mujib wa Waziri Mgimwa, Serikali kuondoa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwa viwanda vinavyozalisha nguo kwa kutumia pamba inayolimwa nchini.
 “Tumeikubali hiyo hoja, tunaifanyia kazi” amelieleza Bunge na kubainisha kwamba, uamuzi huo utasaidia kuongeza ajira nchini na mapato ya wananchi.
Amesema, Serikali inafanya uchambuzi wa suala hilo ili kuona ni wapi itafidia , nakwamba, itatoa ufafanuzi wa jambo hilo katika Muswada wa Fedha wakati wa Mkutano unaoendelea wa Bunge mjini Dodoma.

MATUKIO YA PICHA KUTOKA BUNGENI DODOMA LEO

Waziri Mkuu Mizengo Peter Pinda (kulia) akimsikiliza kwa makini Waziri ujenzi Dkt Jojn Pombe Magufuli(kushoto)(leo) wakati wa kipindi cha maswali na majibu kwenye kikao cha tatu cha mkutano wa nane wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unaoendelea mjini Dodoma.PICHA NA VICENT TIGANYA WA MAELEZO
Naibu Waziri  Ofisi ya Waziri Mkuu , Tawala za mikoa na serikali za Mitaa (TAMISEMI)  Aggrey Mwanri  akijibu maswali mbalimbali yaliulizwa na Wabunge katika kipindi cha maswali na majibu  (leo) mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Chama cha CHADEMA na Msemaji wa Kambi ya Upinzani Bungeni Mh. Freeman Mbowe akimuuliza Waziri Mkuu Mizengo Peter Pinda maswali ya papo kwa papo  (leo) mjini Dodoma katika kikao cha tatu cha mkutano wa nane wa Bunge la Jamhuri ya Muungano unaoendelea mjini Dodoma.
Waziri  wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu ) Stephen Wasira  akiwasilisha Bungeni   (leo) mjini Dodoma taarifa ya hali ya uchumi wa Taifa kwa mwaka 2011 na mwelekeo wa mpango wa maendeleo wa Taifa kwa mwaka wa fedha 2012/13.
Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim  Lipumba  akisikiliza kwa makini taarifa ya hali ya uchumi wa Taifa kwa mwaka 2011 na mwelekeo wa mpango wa maendeleo wa Taifa kwa mwaka wa fedha 2012/13 iliwasilishwa jana (leo)  Bungeni  mjini Dodoma na Waziri wa Nchi  Ofisi ya Rais   (Mahusiano na Uratibu) Stephen Wasira.

CTR YAKUBALI KUHAMISHA KESI YA RYANDIKAYO

Na Ashura Mohamed-Arusha

Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) Jumatano imekubali maombi ya mwendesha mashitaka wa mahakama hiyo ya kuhamishia kesi ya mtuhumiwa wa mauaji ya kimbari ambaye bado anasakwa, Charles Ryandikayo,kwenda kusikilizwa nchini Rwanda, ikiwa kesi ya sita kuhamishiwa nchini humo.
Mahakama iliyotoa maamuzi hayo ikiongozwa na Jaji, Vagn Joensen imeeleza kwamba, kwa kuzingatia hoja zilizowasilishwa na pande zote mbili, imefikia uamuzi wa kuhamishia kesi hiyo nchiniRwanda.

‘’Mahakma imeamua kesi kupelekwa kwenye mamlaka ya Jamhuri yaRwandaili wenye mamlaka hayo kuiwasilisha kesi hiyo mbele ya Mahakama Kuu yaRwandakwa ajili ya kuanza kusikilizwa kwa haraka,’’ inasomeka sehemu ya uamuzi huo.
Imeelezea matumaini yake kwamba’’Jamhuri yaRwanda, kwa kukubali kupokea kesi kutoka mahakama hiyo ya Umoja wa Mataifa, itatimiza wajibu wake kwa uaminifu, uwezo na nia njema ya kuendesha kesi hiyo kwa kufuata viwango vya juu vya haki vya kimataiafa.’
’ 
Ryandikayo ambaye alikuwa Meneja wa mgahawa mmoja wa Mubuga katika wilaya ya Gishyita mkoani Kibuye, Magharibi yaRwandaanashitakiwa kwa mauaji ya kimbari, kula njama za kufanya mauaji hayo, uhalifu dhidi ya binadamu na uhalifu wa kivita.ICTR imeshatoa maamuzi katika maombi matanokamahayo.

Maombi hayo yanahusu mtu mwingine ambayo bado anasakwa pia, Ladislas Ntaganzwa, meya wa zamani wa wilaya ya Nyakizu, mkoani Butare, Kusini mwaRwandana Bernard Munyagishari, anayedaiwa kuwa kiongozi wa wanamgambo wa Interahamwe mkoa wa Gisenyi, Kaskazini ya Rwanda.Lakini upande wa utetezi unatarajiwa kupinga maamuzi hayo.

Maombi mengine matatu ya aina hiyo ambayo yameshatolewa uamuzi na ICTR yanawahusu, Mchungaji Jean Uwinkindi na watuhumiwa wawili ambao nao bado wanasakwa ikiwa ni pamoja na Fulgence Kayishema na Charles Sikubwabo.

Maombi mengine mawili ya aina hiyo ambayo yapo mbele ya mahakama yakisubiri uamuzi ni pamoja na ya Aloys Ndimbati, meya wa zamani wa Gisovu na Luteni Kanali Pheneas Munyarugarama, kamanda wa zamani wa kambi ya jeshi ya Gako, wilayani Kanzenze katika mkoa wa Kigali Vijijini. 

John Mnyika akitoka nje ya Bungeni

Mbunge wa jimbo la Ubungo John Mnyika akitoka nje ya viwanja vya  Bunge la Tanzania jana mjini Dodoma baada ya kukataa kufuta kauli ya kumdhalilisha Rais wa Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania kuwa dhaifu. Mbunge huyo alitoa kauli hiyo wakati akichangia Bajeti ya serikali ya mwaka 2012/13 katika mkutano unaoendelea.Picha na Tiganya Vincent- MAELEZO- Dodoma
Mbunge wa Jimbo la Ubungo John Mnyika akiteta na Mbunge wa jimbo la Wawi Hamad Rashid Mohamed (kushoto) na Mbunge wa Bariadi Mashariki John Cheyo  mara baada ya kuondolewa Bungeni jana mjini Dodoma baada ya kukataa kufuta kauli ya kumdhalilisha Rais wa Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania kuwa dhaifu. Mbunge huyo alitoa kauli hiyo wakati akichangia Bajeti ya serikali ya mwaka 2012/13 katika mkutano unaoendelea.
Mbunge wa jimbo la Ubungo John Mnyika akitoka katika ukumbi wa Bunge la Tanzania jana mjini Dodoma baada ya kukataa kufuta kauli ya kumdhalilisha Rais wa Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania kuwa dhaifu. Mbunge huyo alitoa kauli hiyo wakati akichangia Bajeti ya serikali ya mwaka 2012/13 katika mkutano unaoendelea.

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA KULA CHAKULA CHA JIONI NA VIONGOZI WA UMOJA WA WATANZANIA WAISHIO NCHINI BRAZIL

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza jambo na Katibu wa Umoja wa Watanzania, waishio nchini Brazil, Heri Juma Mbwana, wakati alipokutana nao katika hafla ya chakula cha jioni na mazungumzo, iliyofanyika katika Hoteli ya Arena, Rio de Jeneiro, jana Juni 22, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza jambo na mmoja kati ya wajumbe wa Umoja wa Watanzania, waishio nchini Brazil, , wakati alipokutana nao katika hafla ya chakula cha jioni na mazungumzo, iliyofanyika katika Hoteli ya Arena, Rio de Jeneiro, jana Juni 22, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Mke wa Makam wa Rais, Mama Zakhia Bilal,Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maadhi Juma Maalim, Balozi wa Tanzania nchini Brazil Francis Malambugi, na Balozi Liberata Mulamula, wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Umoja wa Watazanaia, wakati alipokutana nao viongozi hao wa moja wa Watanzania, waishio nchini katika hafla ya chakula cha jioni na mazungumzo, iliyofanyika katika Hoteli ya Arena, Rio de Jeneiro, jana Juni 22, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza Viongozi wa Umoja wa Watanzania, waishio nchini Brazil, wakati alipokutana nao katika hafla ya chakula cha jioni na mazungumzo, iliyofanyika katika Hoteli ya Arena, Rio de Jeneiro, jana Juni 22, 2012. Kulia ni Mama Zakhia Bilal (kushoto) ni Balozi wa Tanzania, nchini Brazil, Francis Malambugi. Picha na Muhidin Sufiani-OMR


SUPER STAR WA NIGERIA OMOTOLA JALADE AKIWA NA WATOTO YATIMA LEO

Mchezaji wa Filamu kutoka nchini Naigeria Omotola Jalade katikati akiwa katika picha ya pamoja na mwigizaji Wema Sepetu kushoto na Khadija Mwanamboka pamoja na watoto yatima wa kituo cha  Tanzania Mitindo House cha jijini Dar es salaam Omotola amekuja nchini maalum kwa ajili ya uzinduzi wa filamu ya Wema Sepetu Super Star ambayo imezinduliwa jana kwenye hoteli ya Hyyat Kilimanjaro jijini Dar es salaam PICHA KWA HISANI YA 8020FASHION
Omotola Jalade akiwasiloi kituoni hapo leo

Omotola Jalade na Wema Sepetu wakiwa katika picha ya pamoja na watoto yatima wa kituo cha Tanzania Mitindo House.

SHA MASHAUZI APAGAWISHA HOLLAND


Msanii wa muziki wa mwambao wa pwani bidada Isha Mashauzi jana
katika mji wa Den Haag nchini Holland alikonga nyoyo za mashabiki
zake pale alipowapa mashauzi yake mashabiki wake.kwa picha zaidi
bonyeza hapa 


WEMA SEPETU AZINDUA FILAMU YAKE YA SUPER STAR

Mwigizaji Wema Sepetu akiingia ukumbini wakati wa uzinduzi wa filamu yake ya Super Star aliyoizindua kwenye hoteli ya Hyyat Kilimanjaro jijini Dar es salaam usiku huu, ikihudhuriwa na watu maarufu pamoja na wanamzuziki na waigizaji, picha zaidi za tukio hili zitawajia baada ya muda
Wema Sepetu akipozi kwa picha mara baada ya kukaa kabla ya kuanza kuchezwa kwa Demo ya filamu hiyo usiku huu kwenye hoteli ya Hyyat Kilimanjaro.
Wageni waalikwa mbalimbali wakishuhudia uzinduzi wa filamu ya Super Star iliyochezwa na mwana dada Wema Sepetu kwenye hotli ya Hyyat Kilimanjaro
Wanamzuiki, watangazaji  pamoja na waigizaji mbalimbali wa filamu walihudhuria katika uzinduzi huo kutoka kulia ni Charles Baba wa Mashujaa Band, Hatman, Mtangazaji Benny Kinyaiya, Mchekeshaji Steve Nyerere, Muigizaj Ramond Kigosi na Richie Mtambalike "Rich Rich" wakishoo Love.
Mwanamuziki Mwinyi ambaye ndiye aliyemvisha pete ya Uchuma Wema Sepetu katika filamu hiyo alikuwepo na yeye
Mtangazaji Dina Marios kutoka Clouds Radio wa tatu kutoka kushoto na kampani yake na wa pili kutoka kulia ni Monica wa Jose Mara.
Waigizaji mbalimbali wakiwa katika uzinduzi huo
Kundi la THT likifanya vitu vyake katika uzinduzi huo
Ankal Michuzi na maiwaifu wake kulia na rafiki yao wakipozi kwa picha
Kulia ni Asma Makau na Dina Marios wakiwa na marafiki zao katika uzinduzi huo.

Maradhi ya Sajuki, laana kwa Steps Entertainment

Nikianzia pale nilipoishia wiki iliyopita ni kwamba zipo sababu nyingi za kuwataka Watanzania wasiione Kampuni ya Steps Entertainment ni rafiki yao. Kile ambacho menejimenti yake imekifanya kwa msanii Juma Kilowoko ‘Sajuki’, kitoshe kuwafanya wakose imani nayo.
Haiwezekani Sajuki awafuate akiwa anaumwa, awaombe msaada wao wamjibu kwamba aende akarekodi filamu, awapelekee waiuze ndiyo zipatikane fedha za kumsafirisha kwenda India kwenye matibabu. Jamani huyu mtu kawafuata anaumwa, hali yake haijifichi, anaumwa kweli lakini kajibiwa hivyo.
Tuone sasa umoja wa wasanii. Nangoja kusikia misimamo ya Vincent Kigosi ‘Ray’, Jacob Steven ‘JB’, Single Mtambalike ‘Richie’ na wengine, kuhusu kujiondoa Steps kutokana na kile ambacho amefanyiwa Sajuki. Ni hatua muhimu kama watafanya hivyo, kwani watakuwa wameitetea tasnia.
Kinyume chake itakuwa ni unafiki. Usaliti, ubinafsi, kuendekeza njaa na kusahau utu. Leo lipo kwa Sajuki, hakuna kati yetu anayejua nani kesho atakuwa mgonjwa pengine kuliko huyo mwenzetu. Kama ndivyo, basi hatutakiwi kupandisha mabega, kwani tafsiri ya kesho ipo kwa Mungu peke yake.
Haishindikani kufanya kazi na makampuni mengine. Inawezekana pia kwa umoja wenu mkaanzisha mtandao wa kusambaza na kuuza kazi zenu. Hili litawapa heshima kubwa kwa kujikomboa, vilevile kushiriki kwa ari na nguvu kupambana na udhalilishaji aliofanyiwa mwenzao.
Hili si la kupuuza, kuna leo na kesho. Usingoje nawe likufike ndiyo ufundishwe kwa mtindo wa kusutwa. Kwamba umeona sasa, enzi zile alipofanyiwa Sajuki uliona sawa, leo yamekufika na wewe ndiyo unaumia. Ni tahadhari tu kwa sababu hii dunia hatuimiliki, kwa hiyo hatuna budi kutendeana haki.
Maisha yetu na tafsiri ya mkate wa kila siku ni mtihani, hivyo kugoma kupeleka kazi Steps inawezekana ni jambo zito. Kama ndivyo, basi tuone kauli zenu za kuonesha kuchukizwa na uamuzi wa kampuni hiyo dhidi ya Sajuki. Toeni sauti basi, mkikaa kimya tutawaona waoga, wazandiki, wanafiki msiojali utu mbele ya fedha.
Tatizo la Steps baada ya kulitazama katika muktadha mpana ni upungufu wa utu mbele ya fedha. Hivyo, hata wasanii watakaokubali kuendelea kufanya kazi na kampuni hiyo, watakuwa hawana ubinadamu. Kwa maana wao wapo radhi mwenzao atoswe, anyanyaswe na kadhalika bila wao kuguswa kwa chochote.
Mimi siyo mtabiri lakini ukweli ukae kwenye kipimo chake kwamba historia itawahukumu. Taadhira na manyanyaso aliyofanyiwa Sajuki haviwezi kupita kimya. Ray na wenzako, zindukeni leo, semeni hapana kwa hili alilotendewa Sajuki. Mafanikio mtayaona hapa duniani na kesho ahera.
Steps imejitengenezea sifa mbaya. Leo hii Sajuki ana mtoto, atakapokua na kujua baba yake aliambiwa afanye kazi ndiyo apate fedha za matibabu wakati hajiwezi, chuki itakaa na akiwa mtu wa kinyongo, ataieneza kwa kizazi chake chote. Namuombea sana maisha marefu Sajuki.
Wakati unasoma makala haya, pengine picha za aina tofauti zinaweza kuingia kichwani kwako na kutoka lakini kubwa ni moja tu, Sajuki anaumwa, yupo dhoofu, anahitaji kusaidiwa lakini wenye upungufu na utu, wamemwambia aende akafanye kazi. Eti, asiporekodi filamu atakufa na maradhi yake.
Ni kwa nini Steps wasingewekeza kwa Sajuki, wakampeleka India kwenye matibabu? Mbona baada ya kupona angefanya kazi nzuri, tena kwa umakini mkubwa? Hapo bila shaka angekuwa na shukurani nyingi juu ya Steps, kwa hiyo angefanya kazi yake yenye nguvu ili kulipa fadhila.
 Sajuki anaumwa, tena anaumwa hasa. Anahitaji msaada wa hali na mali ili atibiwe na kurejea kwenye afya yake. Naomba nisisitize, msanii huyo anaumwa kwelikweli na anahitaji matibabu ya haraka. Fedha zinahitajika akatibiwe India. Huko ndiko kwenye tiba yake.
Pamoja na moyo wa kujitolea ambao mtu yeyote anaweza kuwa nao, hivyo kumchangia kama siyo kumuwezesha Sajuki kwenda India kutibiwa, Steps ilipaswa kuwa ya kwanza, ama kwa kumchangia au kuwezesha safari ya nchi hiyo. Leo tungekuwa tunazungumza mengine lakini thubutu!
Nasema Steps ilipaswa kuwa ya kwanza kwa sababu yenyewe ndiyo inayouza filamu za Sajuki. Kampuni hii inajua matunda ya msanii huyo. Angalau ingefanya hivyo kuonesha namna ilivyoguswa na matatizo ya ndugu yetu. Kama sivyo hivyo, basi uungwana tu.
Steps wanatambua kwamba Sajuki anaumwa lakini wamemfanyia vitendo vya uvunjifu wa haki za binadamu. Wamemtesa kwa kumtumikisha kazi ilhali wanatambua kwamba anaumwa. Tena maradhi ambayo yanahitaji utulivu na faraja. Jamani Sajuki anaumwa, tuache utani, tumuombee, tumchangie akatibi

UWOYA, JANET HAPATOSHI

Na Musa Mateja
Skendo ya matumizi ya dawa za kulevya imesababisha mastaa wawili wa filamu za kibongo, Irene Pancras Uwoya na Janet Mathias kuingia kwenye bifu zito na sasa hapatoshi huku kila mmoja akianika siri nzito za mwenzake, Risasi Jumamosi linafunguka.
Wiki mbili zilizopita, Uwoya ndiye aliyekuwa wa kwanza kufunguka kupitia gazeti hili kuwa alifikia hatua ya kusitisha urafiki wake na Janet kwa madai kuwa alikuwa na skendo hiyo.
UWOYA AIBUA SKENDO
Katika mazungumzo yake yaliyokuwa hayaandikiki gazetini, Uwoya alimsiliba Janet kwa kuanika siri zake nzito, jambo ambalo lilimpandisha hasira msanii huyo na kujikuta naye akimjibu kwa kumchana kama yeye alivyofanya.
Muda mfupi baada ya Uwoya kumwanika, Janet alizama mtandaoni akamlipua mwenzake kuwa alikuwa akiishi naye nyumbani kwao lakini ilishindikana kwa kuwa alikuwa ‘anabwia unga’.
HUYU HAPA JANET
“Huyo anayejiita…(tusi) Irene Uwoya hawezi kuniharibia jina langu kwenye jamii. Anasubiri nikiwa nje ya nchi ndiyo anaanza kusambaza habari mbaya zinazonihusu. Kwa nini asinitafute uso kwa uso?,” ilisomeka sehemu ya mapigo ya Janet ambayo alithibitisha kuwa yanapatikana kwenye ukurasa wake.
UWOYA NAYE
Kwa upande wake, Uwoya alipopatikana tena, alisisitiza kuwa anachofanya Janet ni kumchafua katika jamii kwa vile yeye ni mtu anayeheshimika. Akasema kuwa kamwe hawezi kutumia unga.
HUKO NYUMA
Uwoya na Janet ni marafiki wa siku nyingi ambao walianza kutibuana hivi karibuni baada ya Janet kuingia kwenye filamu akidaiwa kupindua ndoa ya mwenzake.

Kanisa la ajabu

Haruni Sanchawa na George Kayala
WAKATI imezoeleka kwamba makanisa mengi hukusanya waumini kila Jumamosi, Jumapili achilia mbali siku za katikati ya wiki, Risasi Jumamosi limegundua kanisa ambalo waumini wake wanaishi nje ya nchi na huja kila Desemba 24 kwa ajili ya ibada moja tu.
Kanisa hilo lililopo Mbuyuni, Kata ya Wazo Mtaa wa Salasala, Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, inadaiwa kuwa waumini wake wanatokea Ugiriki wakiwa ni Wakristo wa madhehebu mbalimbali.
Habari zinasema kuwa kuna Wakatoliki, Walokole na Waanglikana ambao husali pamoja katika kanisa hilo.
“Wakishafanya ibada yao ya Sikukuu ya Krismasi hurudi kwao na kanisa hufungwa mpaka mwaka unaofuata,” kilisema chanzo chetu kimoja.
Mbali ya milango ya kanisa hilo kufungwa baada ya waumini hao kuondoka lakini kuna mtu anayefanya usafi kwa ajili ya kulitunza kanisa hilo.
Pia, askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ambao hufanya shughuli zao karibu na sehemu lilipo kanisa hilo, huchangia kuliwekea ulinzi saa nyingine bila kujitambua.
Waandishi wa gazeti hili walipofuatilia, walibaini kuwa linamilikiwa na mwanamke wa Kigiriki aliyefahamika kwa jina moja la Stella (70). Pia, ilifahamika kuwa awali, kanisa hilo lilikuwa likimilikiwa na raia wa Kigiriki aitwaye Mitili ambaye alipofariki dunia aliwaachia urithi wanae wawili ambapo mmoja wao ni Stella.
Jitihada za waandishi wetu kuzungumza na Stella ziligonga mwamba baada ya kuambiwa amesafiri kwenda Ugiriki.
Risasi likapiga kiguu na njia hadi kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Salasala, Kayenge Mshindo ambaye alishangaa na kusema kuwa hajui chochote kuhusiana na kanisa hilo, akaomba apewe muda wa kulifanyia kazi.

VIONGOZI WA MAKANISA WANASEMAJE?
Baadhi ya viongozi wa makanisa, walizungumza na gazeti hili kuhusu uwepo wa kanisa hilo linaloonekana kuwa la ajabu.
Wa kwanza alikuwa ni Nabii Flora Peter kiongozi wa Kanisa la Maombezi Mbezi Beach jijini Dar, ambaye alivitaka vyombo vya usalama kulifanyia kazi suala hilo.
Naye, Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel  Fellowship, Zachary Kakobe, alisema hana cha kuzungumzia kwani kila kukicha watu wanaanzisha makanisa.
Mchungaji wa kanisa la Assemblies of God, Getrude Rwakatare lilipo Mikocheni B, Dar alisema kuwa kanisa hilo halijui lakini kama lipo serikali ifanyie uchunguzi kwa ajili ya usalama wa taifa.
Kiongozi wa Kanisa la Living Water Center, Mtume Onesmo Ndege: “Hilo siyo kanisa kwani haiwezekani waumini wakawa wanaabudu mara moja kwa mwaka, isipokuwa ni dini ya kundi la watu wachache na wanajua nini wanachokiabudu.”
Kiongozi wa  Kanisa la Christian Mission  Fellowship, Mchungaji Antony Lusekelo ‘Mzee wa Upako’: “Sijui chochote kuhusu kanisa hilo lakini Watanzania wanatakiwa kuwa macho katika kipindi hiki ni cha nyakati za mwisho.”

FREEMASON...TANZANIA

Na Mwandishi wetu
HEKAHEKA ya wimbi la mastaa wa Bongo kutumika kwenye imani inayodaiwa kuwa ni ya kishetani duniani maarufu kwa jina la Freemason a.k.a Wajenzi Huru inazidi kuchukua nafasi kwa kasi baada ya hivi karibuni kudaiwa kuwa, staa wa sinema za Bongo, Jacqueline Wolper Massawe naye ametumbukia humo, Risasi Jumamosi limesheheni.
NI NCHINI AFRIKA KUSINI
Kwa mujibu wa chanzo cha uhakika, Wolper ameinamisha kichwa na kumwagiwa maji ya imani hiyo kama ishara ya kujiunga nchini Afrika Kusini, mapema mwaka huu.
NANI SHAHIDI?
Mmoja wa marafiki wa Wolper aliliambia gazeti hili kwamba, Wolper alishawishiwa na msanii mwingine wa kiume wa filamu Bongo ambaye hana jina kubwa kuwa ndiye aliyempa namba za mawasiliano za wahusika nchini Afrika Kusini.
“Wolper ameingia Freemason na aliyemshawishi ni msanii ….(anataja jina), yeye alimwambia akiwa huko anaona matunda yake kwani ni imani ambayo binadamu unaishi kama peponi,” alisema rafiki huyo.
UTAJIRI WA HARAKA WATAJWA
Kwa mujibu wa chanzo hicho, tangu Wolper amejiunga na imani hiyo inayosambaa kwa kasi nchini Tanzania amekuwa akipata mafanikio makubwa tena kwa haraka.
“Wee kama unataka kuamini, angalia tangu mwaka huu (2012) umeanza, Wolper mambo yanamyookea tu. Awali alikuwa akiishi eneo ambalo halimfai kama staa, sasa amehamia Mbezi, tena kwenye jumba zuri sana,” alisema mtoa habari huyo.
Aliendelea kuweka wazi kuwa, magari na miradi mingine aliyonayo si ofa kutoka kwa mchumba wake aitwaye Abdallah Mtoro ‘Dallas’ kama anavyodai mwenyewe Wolper bali ni ‘baraka’ ya Freemason.
Akasema: “Mmekuwa mkiandika eti kanunuliwa magari na mchumba wake, nani kasema? Ile ni kama njia ya kukwepea tu, lakini ukweli ni kwamba Freemason ndiyo wanambeba kwa sasa.”
Akaongeza: “Wazazi wa Wolper wapo katika wakati mgumu, mama yake amepata fununu za mwanaye kujiunga na Freemason na ndugu wakamweka chini kumwonya kama ni kweli ajitoe mara moja.”

KANUMBA ALIJIUNGIA NIGERIA
Hivi karibuni, mtu mmoja aliyejitaja kuwa ni mchungaji wa kanisa moja la kiroho jijini Dar, George Kariuki alizungumza kupitia Kituo cha Radio Times FM na kudai kuwa marehemu Steven Kanumba alijiunga na u-Freemason nchini Nigeria, nchi ambayo iko mbali kidogo kutoka Tanzania kuliko ilivyo Afrika Kusini anakodaiwa kwenda Wolper.
Hata hivyo, matokeo ya Kanumba kujiunga yalionekana, kupata mali kwa kasi ya ajabu, nyota yake kung’ara lakini mwisho wa yote ilifika mahali imani hiyo inatajwa na baadhi ya watu kuwa ndiyo chanzo kikuu cha kifo chake (Mungu amlaze pema peponi-amina).

BOFYA HAPA UMSIKIE WOLPER
Baada ya madai hayo, Risasi Jumamosi lilimsaka Wolper kwa nguvu zote na kubahatika kukutana naye siku ya Jumatano maeneo ya Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Baada ya salamu, msanii huyo mwenye aibu kwa mbali, alisomewa ‘mashitaka’ yake yote huku akiwa amemkazia macho paparazi.
Wolper: “Mh! jamani, mnajua haya mambo bwana yana siri kubwa ndani yake. Wako watu wanatajwa ni Freemason, wengine wapo lakini hawatajwi, ni kwa nini?”

WOLPER JIBU SWALI
Paparazi: “Labda kikubwa ungetuambia ni kweli upo huko au si kweli?”
Wolper: “Unajua bwana, mimi sina hela kama wanavyosema watu. Na haya yote yametokana na nilivyomsaidia Sajuki (Juma Kilowoko). Yule nilimsaidia kwa sababu niliguswa kutoka moyoni, lakini familia yangu yenyewe ina uhitaji mkubwa sana.
“Tena naomba jamii ielewe kuwa, sina ‘minoti’ ya kumwaga. Napata tabu watu wananifuata wakilia shida zao wakiamini nina fedha kibao, si kweli jamani.”

WOLPER VIPI?
Paparazi: “Umezungumza vizuri, lakini hujajibu suala la kujiunga na Freemason kama ni kweli au si kweli?”
Wolper: “Mimi gari si alininunulia Dallas, mbona nilishasema jamani au?”
Paparazi: “Sawa, ulishasema, vipi kuhusu Freemason sasa?”
Wolper: “Ni kwa sababu ya hizi nguo au? Maana nguo navaa bila kujua alama zake, sasa kama kuna za Freemason mimi nitajuaje jamani, ee?”

HAYA SASA
“Ila labda nikiri kitu kimoja, ni kweli niliwahi kuitwa na watu wakaniambia nijiunge kwenye imani hiyo, waliniahidi kwamba nikikubali maisha yangu yatakuwa mazuri na ulinzi wa afya yangu.”
Paparazi: “Ina maana hujajiunga unafikiria kwanza?”
Wolper: “We unaonaje, nijiunge au? Mimi sitaki nasikia wengi wameingia wanafanikiwa kwa kasi.”

MASWALI YA MHARIRI
Kama kweli Wolper si Freemason, amejuaje mavazi yake yana alama ya imani hiyo? Kwa nini anaomba ushauri huku anasema haitaki imani hiyo?  Risasi Jumamosi linaendelea kumfuatilia kwa karibu kuhusu shughuli zake za

WATANZANIA

WATANZANIA BADO WANA KIDONDA KINACHOUMA KWA KUUZWA NYUMBA ZA SERIKALI KWA BEI YA KUTUPWA

KAMA ilivyo ada tuanze makala haya kwa kumuomba Mungu atuzidishie siku za kuishi hapa duniani kwani akiamua kutunyang’anya pumzi, tunakwisha wote, hivyo basi inatupasa kumshukuru na kufuata mafundisho yake ambayo yanasisitiza upendo, amani na kumcha yeye.
Baada ya kutamka hayo tuingie katika mada ya leo, Wahenga walisema msema kweli ni mpenzi wa Mungu nami leo nataka niseme kweli kabisa kutoka rohoni.

Nilipata faraja sana wiki mbili zilizopita baada ya kumsikia Mbunge wa Simanjiro, Christopher ole Sendeka akisema  bungeni  Dodoma mwezi uliopita, kwamba anakusudia kuwasilisha hoja binafsi katika kikao kijacho cha Bunge cha Aprili mwaka huu, kulitaka Bunge lipitishe azimio la kurudishwa kwa nyumba za Serikali zilizouzwa katika mazingira ya kutatanisha na serikali ya awamu ya tatu iliyokuwa ikiongozwa na Benjamin William Mkapa.

Mheshimiwa Sendeka ambaye anajipambanua kuwa ni  mmoja wa wabunge ambao wanapambana na vitendo vya ufisadi nchini, akasema hatua hiyo ya serikali kuuza nyumba za watumishi wake haikubaliki siyo tu kwa sababu siyo endelevu, bali pia ina kila dalili za ukiukwaji wa misingi ya uadilifu na utawala bora lakini pia namuongezea kuwa wananchi ambao ndiyo wenye mali hawakushirikishwa.

Ndugu zangu, nasema wazi kuwa kauli ya Mheshimiwa Sendeka  hapana shaka itakuwa imewafariji Watanzania wengi ambao bado wana kidonda na maumivu kwa kuuzwa nyumba hizo za serikali kwa bei ya kutupwa, wananchi hao  walidhani hawana  mtu wa kupigania nyumba hizo za serikali ambazo si mali za fulani bali ni za wananchi wote wa nchi hii.

Nimuambie ole Sendeka kuwa  wananchi wengi wako nyuma yako na wale ambao nawafahamu na nisiowafahamu ambao  walipinga kwa nguvu zote pasipo mafanikio kitendo cha serikali kuuza nyumba hizo, wanakuombea maisha marefu ili azma yako itimie.

Hakuna ambaye hakumbuki kwamba uuzwaji wa nyumba hizo ulipingwa vikali katika kila kona ya nchi yetu siyo tu kwa kuwa ziliuzwa kwa bei ya kutupwa au ya kupasiana kama mpira wa miguu au wa mikono, bali pia zoezi hilo kuna madai kuwa lilifanyika bila kuwa na uwazi na kutofuatwa kwa taratibu zilizowekwa kuhusu uuzwaji wa mali za serikali. Hii ni mbaya sana kwa taifa linalosisitiza amani na mshikamano wa kitaifa.

Wananchi wengi walitafsiri kuwa kwa kuwa walipinga uuzwaji wa nyumba hizo za umma basi wakasema kwamba uuzwaji wa nyumba hizo ulionekana dhahiri kufanywa kibabe. Inawezekana uuzwaji wa nyumba hizo bila shaka ulipata baraka za Baraza la Mawaziri, lakini  kitendo kile tunaweza kutafsiri kwamba kilikuwa ni unyang’anyi na ukwapuaji wa wazi wa mali ya umma kinachoweza kufananishwa na usaliti kwa watu wanaotajwa na katiba kuwa ndiyo wanaoiweka serikali madarakani.

Nasema hivyo kwa sababu viongozi wa serikali ambao ndiyo waliokuwa na dhima ya kulinda mali hiyo ya umma,  waliugeuka umma wa Watanzania, walikaa na kula njama za kujigawia nyumba hizo  ambazo zilijengwa sehemu maalumu katika miji yote nchini ili kuwawezesha viongozi wa serikali kuishi karibu na sehemu zao za kazi kwa lengo la kuleta ufanisi katika utendaji wa kazi zao za kila siku.
Hakika tumuunge mkono Mheshimiwa Sendeka na niseme tu kwamba makala haya hayatoshi kuorodhesha madudu yote yaliyotokana na kitendo hicho ambacho kilichofanywa na viongozi wetu. Ni dhahiri huo ni ufisadi mkubwa.

Hata hivyo, kitendo kile tunaweza kukitafsiri kwa lugha nyepesi kwamba waliofanya vile walitenda kitendo kibaya sana si kwa usalama wa nchi tu bali pia kwa masilahi ya umma na wengine waliochukizwa na uuzajwi ule walisema uuzwaji huo ulifanyika katika staili ya chukua chako mapema na pengine ndiyo sababu nyumba hizo baada ya kuuzwa kwa viongozi wa serikali siku chache baadaye ikagundulika kuwa zinamilikiwa na watu ambao siyo wa serikali kama alivyosema Mheshimiwa Sendeka.

Mheshimiwa Sendeka ambaye ana hoja inayoungwa mkono na  Watanzania wengi sana  ni kwamba uuzwaji huo haukuwa halali, bali ulikuwa ni wizi wa mchana kweupe na waliofanya vile hawakuwa na hata chembe ya huruma kwa taifa na wananchi wake.
 Wananchi wangeweza kulia na wabunge kama wizi huo ungekuwa umeidhinishwa na Bunge ambalo mamlaka yake yanatokana na wananchi wenyewe lakini waliofanya kitendo kile, hata wabunge hawakuwashirikisha kwa sababu walijua kuwa wangegonga mwamba. Hakuna mbunge ambaye angekubali kuidhinisha wizi huo.

Kitendo cha wateule wachache serikalini kukaa na kula njama za kujigawia nyumba za umma, hakika hakielezeki hata kidogo kama ambavyo hakikubaliki kwa namna yoyote ile na ndiyo maana natoa wito kwa wananchi na hasa wabunge wote kuwa hoja hiyo itakapoletwa bungeni iungwe mkono na wabunge wengi bila kujali itikadi ili walionunua wanyang’anywe.

Yapo madai kuwa viongozi walionunua nyumba hizo, kabla ya kununua walikula njama na kuzikarabati kwa kutumia mamilioni ya fedha za serikali kisha kugawiana kama pipi huku wakijua kuna serikali ya awamu nyingine inakuja na itahitaji watumishi wake waishi humo. Matokeo yake mawaziri, majaji na maofisa wengine wakafikia mahotelini ambapo serikali ililipa mamilioni ya shilingi kama siyo mabilioni.

Bila aibu wala woga, hata nyumba zilizokuwa nyeti kama za  mawaziri; makatibu wakuu; wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya; maafisa usalama wa taifa; makamanda wa polisi wa mikoa na wilaya; mahakimu na majaji; na wakuu wengine muhimu ziliuzwa kwa bei ya ‘kutupa’. Nyingi ya nyumba hizo zilikuwa sehemu nyeti kama vile karibu na vituo vya polisi au majengo ya vyombo vya ulinzi na usalama au karibu na boma au wizara.   

Ndugu zangu wote tulishuhudia  viongozi walioteuliwa na serikali ya Awamu ya Nne ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete, walijikuta hawana pa kuishi hivyo kulazimika kukodishiwa mahoteli ya kifahari kama vile nchi hii ni tajiri sana hapa duniani.
 Kwa mfano, Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha aliripotiwa kuishi katika hoteli moja jijini Dar es Salaam na kulipiwa Shilingi milioni 60 kwa mwezi lakini hata wakati serikali ya awamu hii inaanza, mabilioni ya shilingi yalitumika kuweka mawaziri na majaji kwenye mahoteli. Huu ni wizi wa mchana.

Mimi naamini na Watanzania wakiongozwa na wabunge  wenye nia thabiti ya kulinda rasilimali za nchi hii kwa faida ya raia wa sasa na vizazi vijavyo, wataunga mkono hoja binafsi ya Mbunge Sendeka atakapoiwasilisha bungeni.

Wakati Mheshimiwa Sendeka akijiandaa, sisi tulio nyuma yake kwa umoja wetu tuzidi kupiga kelele kupinga uuzwaji wa nyumba hizo hadi zitakaporudishwa serikalini na ikiwezekana wahusika waadhibiwe. Walitumia vibaya sana ofisi za umma, naamini wakijifungia katika vyumba na kutafakari watagundua kuwa walichokifanya ni ubinafsi uliokithiri na kutojali wananchi waliowaweka madarakani.
Jipu limepasuka, siwezi kuwa adui kwa kusema ukweli.